Mfuko hautazalisha vitambulisho halisi. Wanufaika waliotimiza umri wa miaka 18 na wenye namba za NIDA watazitumia kupata huduma vituoni. Aidha kila mnufaika atapewa namba ya kitambulisho ambacho kitatolewa kama nakala tepe (soft copy) na kuitumia kupata huduma katika kituo kilichosajiliwa na Mfuko.
Mwananchi anayetaka kujisajili kupitia vifurushi vya Ngorongoro Afya na Serengeti Afya halazimiki kufika ofisi za Mfuko. Anaweza kujihudumia kwa njia ya mtandao kupitia NHIF Self Service inayopatikana katika  https://selfservice.nhif.or.tz .Ili kuingia katika mfumo wa usajili mwanachama anapasw...
Mtoto mmoja mmoja kwenye Kaya zisizo na uwezo ambazo zimetambuliwa na Mpango wa TASAF pamoja na TAMISEMI wataingizwa kwenye mfumo maalum wa Bima ya Afya kwa wote. Hivyo nao watapata matibabu kupitia mfumo huo. Kwa wananchi wenye kipato cha kawaida wanaweza kuchangia kidogo kidogo kwa kudunduliza.
Ndiyo. Baada ya kukamilisha usajili Mfuko utatuma kiwango stahiki cha huduma kwa kila mnufaika kupitia namba ya simu iliyotumika wakati wa usajili. Kiwango cha ukomo kitajumuisha huduma za matibabu ya nje (outpatient) na huduma za kulazwa (inpatient). Aidha Mfuko utatuma ujumbe kila mwanachama anapo...
Mfuko hautazalisha vitambulisho halisi, hivyo wanufaika wa Toto Afya watapewa namba ya kitambulisho au nakala tepe (soft copy) ya kitambulisho watakayotomia katika vituo vya kupata huduma vilivyosajiliwa nwa Mfuko nchi nzima.
Ndiyo. Watoto wanaosajiliwa kupitia makundi (shule) michango yao ni Shilingi 50,400 kwa mwaka, hawatakuwa na muda wa kusubiri kabla ya kunufaika na huduma zao zinaanza muda mmoja na kuisha kwa wakati mmoja. Watoto wanaosajiliwa mmoja mmoja watakuwa na muda wa siku 90 kusubiri kupata huduma, watakuwa...
Hapana. Mzazi/Mlezi/Mdhamini halazimiki kuwa mwanachama wa mfuko wakati wa usajili mtoto katika Mfuko kupitia kifurushi cha mtoto mmoja mmoja. Hata hivyo inamlazimu mzazi/mlezi kujaza taarifa za mtoto na kusaini kwa niaba ya mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18.
Hapana. Mzazi/mlezi anayetaka kumsajili mtoto wake anaweza kufanya hivyo kwa kufika ofisi ya Mfuko, au kujihudumia mwenyewe kupitia mfumo wa NHIF self service https://selfservice.nhif.or.tz. Aidha Mfuko utateua Mawakala wa Usajili ambao watakuwa ni Mabenki, na Mitandao ya Simu kufanya usajili wa wan...
Kwa watoto wanaosajiliwa kwa makundi, usajili wao unafanywa na shule husika ambapo wanahitaji kuwa na picha moja ya passport pamoja na namba ya usajili shuleni. Watoto wanaosajiliwa mmoja mmoja watahitajika kuwa na picha ya passport, namba ya uhakiki wa cheti cha kuzaliwa inayotolewa na RITA ambapo...
Watoto wanaosajiliwa katika makundi kupitia shule mchango ni Shilingi 50,400 kwa kila mtoto kwa mwaka. Endapo mtoto atasajiliwa peke yake mchango kwa mwaka utakuwa Shilingi 150,000.  Michango yote ya uanachama inalipwa moja kwa moja katika akaunti ya Mfuko kwa kutumia control namba