Utaratibu wa kusajiliwa katika vifurushi vya Ngorongoro Afya na Serengeti Afya ni upi?
Utaratibu wa kusajiliwa katika vifurushi vya Ngorongoro Afya na Serengeti Afya ni upi?
Mwananchi anayetaka kujisajili kupitia vifurushi vya Ngorongoro Afya na Serengeti Afya halazimiki kufika ofisi za Mfuko. Anaweza kujihudumia kwa njia ya mtandao kupitia NHIF Self Service inayopatikana katika https://selfservice.nhif.or.tz .Ili kuingia katika mfumo wa usajili mwanachama anapaswa kuwa na umri wa miaka 18. Endapo atasajili mwenza na wategemezi watoto chini ya umri wa mika 21, atahitaji kuwa na namba ya uhakiki wa vyeti vya ndoa pamoja na vyeti vya kuzaliwa watoto kutoka RITA. Aidha inahitajika picha ya kila mnufaika atakayesajiliwa ambayo itaingizwa kupitia mfumo uliotajwa hapo juu.