Je, ni lazima kufika ofisi za Mfuko kufanya usajili wa mtoto mmoja mmoja?

Hapana. Mzazi/mlezi anayetaka kumsajili mtoto wake anaweza kufanya hivyo kwa kufika ofisi ya Mfuko, au kujihudumia mwenyewe kupitia mfumo wa NHIF self service https://selfservice.nhif.or.tz. Aidha Mfuko utateua Mawakala wa Usajili ambao watakuwa ni Mabenki, na Mitandao ya Simu kufanya usajili wa wanachama wake. Orodha ya mawakala hao itatangazwa katika tovuti ya Mfuko na kurasa rasmi za Mfuko za mitandao ya kijamii;