Wanachama wa vifurushi vya Ngorongoro Afya na Serengeti Afya watatambuliwaje katika vituo vya kutolea huduma?

Mfuko hautazalisha vitambulisho halisi. Wanufaika waliotimiza umri wa miaka 18 na wenye namba za NIDA watazitumia kupata huduma vituoni. Aidha kila mnufaika atapewa namba ya kitambulisho ambacho kitatolewa kama nakala tepe (soft copy) na kuitumia kupata huduma katika kituo kilichosajiliwa na Mfuko.