Je, ni lazima mzazi/mlezi awe mwanachama ili kumsajili mtoto kupitia kifurushi cha Toto Afya ya mmoja mmoja?

Hapana. Mzazi/Mlezi/Mdhamini halazimiki kuwa mwanachama wa mfuko wakati wa usajili mtoto katika Mfuko kupitia kifurushi cha mtoto mmoja mmoja. Hata hivyo inamlazimu mzazi/mlezi kujaza taarifa za mtoto na kusaini kwa niaba ya mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18.