Je, kutakuwa na ukomo wa huduma kwa kundi la Toto Afya?

Ndiyo. Baada ya kukamilisha usajili Mfuko utatuma kiwango stahiki cha huduma kwa kila mnufaika kupitia namba ya simu iliyotumika wakati wa usajili. Kiwango cha ukomo kitajumuisha huduma za matibabu ya nje (outpatient) na huduma za kulazwa (inpatient). Aidha Mfuko utatuma ujumbe kila mwanachama anapotumia kadi yake kituoni na kuonesha kiasi kilichobakia. Hivyo wanufaika wanapaswa kuepuka matumizi holela ya vitambulisho vyao ili kuwa na uhakika wa matibau mwaka mzima.