Ninajisikia heshima kukukaribisha kwenye tovuti hii ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Tovuti hii inatoa taarifa mbalimbali zinazohusu Mfuko hususan uendeshaji wake. Umuhimu wa tovuti hii, pamoja na mambo mengine, ni kuwezesha upatikanaji wa taarifa kati ya Mfuko na wanufaika wake, wadau mbalimbali na umma kwa ujumla. Kwa kuongezea, inafanya kazi ya kutanua fursa za kuwafikia watu wengi zaidi ndani nan je ya nchi.
Taarifa zilizopo kwenye tovuti hii zinalenga kuboresha huduma kwa wateja kupitia jukwaa la mtandaoni ambalo linaonyesha huduma mbalimbali Mfuko na kupokea maoni ya wateja. Tovuti hii inatambulika kama mojawapo ya njia bora ya mawasiliano ya Mfuko.
Katika tovuti hii pia utapata taarifa za matukio mbalimbali ya Mfuko, unaweza kupakua nyaraka mbalimbali na taarifa kuhusu matukio mbalimbali yanayotarajiwa kufanyika. Lakini pia mdau anaweza kupata fomu za uanachama na kupata taarifa zote muhimu kwa ajili ya usajili.
Kwa kuwa Mfuko una mkakati wa shirika wa kuhakikisha kufikia malengo ya Bima ya Afya kwa Wote, Mfuko huo unatanua wigo wake wa uanachama ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za bima ya afya kwa kila mwananchi. Tunaahidi kuendeleza shughuli za uhamasishaji na uelimishaji wa umma kwa kutangaza Mfuko kupitia njia tofauti, hii ikiwa mojawapo. Hata hivyo, tunapowasiliana na wadau wetu kupitia mtandao, tunaendelea kuwakaribisha kupata huduma kupitia ofisi zetu.
Baada ya kusema haya, natumai tovuti hii itakuwa ya manufaa kwako, rahisi kutumia na ya kuvutia. Iwapo utashindwa kupata unachotafuta, tafadhali tujulishe kupitia anwani mbalimbali zinazopatikana katika tovuti hii na tutakusaidia.
Karibu sana.
Dr. Irene C Isaka
MKURUGENZI MKUU
MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA