NHIF na NMB wakutana kwa majadiliano ya kimkakati

Imewekwa: 16 July, 2025
NHIF na NMB wakutana kwa majadiliano ya kimkakati

16 Julai, 2025 Dodoma

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dkt. Irene C. Isaka, amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Benki ya NMB wakiongozwa na Bw.William Makoresho ambaye ni Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa Taasisi za Serikali.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Isaka alielezea hatua mbalimbali zinazofanywa na Mfuko kwenye utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, ambapo pande zote mbili zilijadiliana namna ya kushirikiana kutimiza adhima hiyo. Kwa upande wa Benki ya NMB, Bw. Makoresho ilielezea nia ya Benki hiyo kutoa mikopo kwa vikundi mbalimbali ikiwemo wakulima, wavuvi, wafugaji na makundi mengine, mikopo itakayowezesha kulipia bima ya afya kwenye Mfuko wa NHIF, ili makundi hayo yawe na uhakika wa matibabu.

Ili kuhakikisha makubaliano hayo yanafikiwa, pande zote zimekubaliana kuunda timu ya wataalam, kupitia masuala yaliyojadiliwa na kuandaa mapendekezo  ya utekelezaji kwa mapitio ya Menejimenti za Mfuko na Benki.

Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ukiongozwa na DKT.Irene Isaka wa pili kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja  baada ya majadiliano na uongozi wa NMB unaoshughulikia masuala ya watumishi wa Umma ukiongozwa na Bw. Wiliam Makoresho wa tatu kutoka kulia. 

Mazungumzo hayo yalishuhudiwa na Mkurugenzi wa Fedha wa NHIF Bi. Grace Temba, kwa upande wa NMB Bw. Charles Gibure, Meneja Mwandamizi Huduma za Kibenki kwa Taasisi na Bw. Festo Mwakasendo, Meneja Mahusiano Huduma za Kibenki kwa Taasisi walishiriki kikao hicho.

"Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa".