Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philipo Mpango amekabidhi cheti cha kutambua mchango wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika kuwezesha Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
Cheti hicho kilipokelewa jana na Mkurugenzi wa Tiba na Huduma za Kitaalam wa NHIF Dkt. David Mwenesano kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Dkt. Irene C. Isaka.
Mkutano huu umefanyika jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia tarehe 11 hadi 13 Julai,2025 katika ukumbi wa JKCC na kuhudhuriwa na washikiri Zaidi ya 1,500 kutoka katika Halmashauri za Mikoa yote Tanzania.
Katika mkutano huo,NHIF ilifanya wasilisho kuhusu maboresho mbalimbali yaliyofanya hasa kwenye eneo la mifumo ya TEHAMA.
Bima ya afya kwa Wote, Jiunge Sasa