Je kuna tofauti ya Toto Afya kupitia makundi na ya Mtoto mmoja mmoja?
Je kuna tofauti ya Toto Afya kupitia makundi na ya Mtoto mmoja mmoja?
Ndiyo. Watoto wanaosajiliwa kupitia makundi (shule) michango yao ni Shilingi 50,400 kwa mwaka, hawatakuwa na muda wa kusubiri kabla ya kunufaika na huduma zao zinaanza muda mmoja na kuisha kwa wakati mmoja. Watoto wanaosajiliwa mmoja mmoja watakuwa na muda wa siku 90 kusubiri kupata huduma, watakuwa na ukomo tofauti wa huduma na michango yao ni TZS 150,000 kwa mwaka. Aidha watoto wanaosajiliwa mmoja mmoja wanaweza kujiunga na kifurushi cha Ngorongoro Afya au Serengeti Afya kwa kulipa michango ya vifurushi husika. Hata hivyo, watoto wote watahitaji kuzingatia utaratibu wa rufaa katika kupata matibabu.