Je, ni mahitaji gani yanatakiwa ili kumsajili mtoto katika bima ya afya?

Kwa watoto wanaosajiliwa kwa makundi, usajili wao unafanywa na shule husika ambapo wanahitaji kuwa na picha moja ya passport pamoja na namba ya usajili shuleni. Watoto wanaosajiliwa mmoja mmoja watahitajika kuwa na picha ya passport, namba ya uhakiki wa cheti cha kuzaliwa inayotolewa na RITA ambapo mzazi/mlezi atamsajili kupitia mfumo wa NHIF self service unaopatikana kupitia https://selfservice.nhif.or.tz