Utangulizi
Ni Mpango wa hiari ulioanzishwa kwa sheria Na.1 ya mwaka 2001 (Sura 409 ya sheria za Tanzania Toleo la 2002) - pdf CHF ACT (71 KB) wa kaya au familia kuchangia gharama za matibabu kabla ya kuugua. Kaya katika Huduma za Matibabu za CHF ni

  •     Baba, mama na watoto chini ya umri wa miaka 18;
  •     Mtu yeyote mwenye umri zaidi ya miaka 18;
  •     Taasisi, mfano Shule (wanafunzi) Ushirika (wanaushirika),vikundi vya uzalishaji n.k

Sababu za kuanzishwa kwa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF):

  •     Kuiwezesha jamii kumiliki huduma za afya zinazowahusu katika maeneo wanayoishi.
  •     Kushirikisha jamii kutoa mawazo yao ili kuboresha huduma za afya kupitia mikutano na kamati mbalimbali watakazozichagua wao wenyewe.
  •     Kuchangia kwa hali na mali huduma za afya zinazowahusu wananchi katika ngazi ya Kijiji,Kata,Tarafa hadi Wilaya.
  •     Kuboresha huduma za matibabu kupitia utaratibu rahisi na nafuu wa uchangiaji.