Mafao Yatolewayo

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ulianzishwa ili kusimamia upatikanaji wa huduma za matibabu kwa watumishi wa Serikali, Umma, Binafsi, Wanafunzi na makundi mbalimbali ya watu ili kupata huduma za matibabu kupitia vituo vya Serikali, Madhehebu ya dini, Binafsi na Maduka ya Dawa ambayo yamesajiliwa na Mfuko.

WALENGWA WA HUDUMA ZA NHIF

  • Watumishi wa Taasisi za Umma na Serikali,
  • Watumishi wa Sekta binafsi za ajira,
  • Watumishi wa Madhehebu ya dini
  • Madiwani
  • Wanafunzi wa Shule, Taasisi za Elimu na Vyuo vya Elimu ya Juu
  • Watu binafsi

KWANINI UCHAGUE NHIF?

  • Ina mtandao mpana wa vituo vya matibabu zaidi ya 9,000 nchi nzima.
  • Inagharamia matibabu sawasawa kwa wanachama wake wote bila kujali kiasi au kiwango cha uchangiaji.
  • Huduma za matibabu hutolewa kadri ya mahitaji na ushauri wa daktari.
  • Kiwango cha mchango hakiangalii hali ya afya ya mwananchama.
  • Mwanachama ana nafasi ya kusajili wategemezi wake kulingana na taratibu zilizopo.
  • Kadi ya NHIF hutumiwa katika kituo chochote cha afya kilichosajiliwa na NHIF popote Tanzania.
  • Mwanachama mstaafu ana nafasi ya kuendelea kutibiwa na NHIF bila kuendelea kuchangaia kwa kufuata taratibu zilizowekwa.

KITITA CHA MAFAO

Kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kimatibabu, hivi sasa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unalipia huduma zote za kimatibabu kwa wanachama wake.

Mfuko wa Bima ya Afya unatoa mafao yafuatayo kwa wanachama wake:

  • Kujiandikisha na kumwona daktari.
  • Vipimo zaidi ya 350 vya msingi na maalum kama CT-Scan na MRI.
  • Dawa zote zilizosajiliwa na zinazoruhusiwa kutumika hapa nchini.
  • Huduma za kulazwa kwa daraja la kwanza au la pili kulingana na makubaliano kati ya NHIF na Watoa huduma.
  • Upasuaji mdogo, mkubwa na wa kitaalamu.
  • Huduma za afya ya meno
  • Matibabu ya macho.
  • Huduma za mazoezi ya viungo (physiotherapy)
  • Miwani ya kusomea kwa mwanachama mchangiaji
  • Matibabu kwa Wastaafu na wenzi wao
  • Vifaa saidizi (Medical/ Orthopedic appliances) kama Fimbo nyeupe, magongo, vifaa vya usikivu, vifaa shikizi vya shingo, n.k.

HUDUMA ZINAZOHITAJI VIBALI MAALUM

Huduma hizi ni pamoja na:-

  • Kipimo cha MRI na CT-Scan
  • Vifaa tiba saidizi (Orthopaedic Appliances)
  • Huduma ya nyenzo saidizi (Implants)
  • Huduma za miwani ya kusomea kwa mwanachama mchangiaji.

Mwanachama anayehitaji kupata baadhi ya huduma za vibali maalum kwa mara ya kwanza atafunguliwa faili katika ofisi iliyo karibu nae. Atakapohitaji kibali hicho hicho kwa mara ya pili atahudumiwa huko huko hospitali.

Huduma hizi ni pamoja na:

  • Huduma za kusafisha damu (Haemodialysis)
  • Dawa za kuongeza uzalishaji wa damu (Erytrhropoietin)
  • Dawa za Saratani (Chemotherapy)
  • Huduma kwa waliopandikizwa Figo (Immuno-suppressants/ Immuno-stimulants)
  • Huduma za mionzi (Radiation Therapy)
Huduma za upasuaji wa Moyo (Advanced Cardiac Services)