Ushirika Afya
Ushirika Afya ni mpango mahsusi ulioanzishwa na Mfuko kwa lengo la kuwasajili wakulima wa mazao ya kimkakati kama vile Korosho, Pamba, Kahawa na Chai. Wanachama hawa ni wale waliosajiliwa katika vyama vya msingi vya ushirika wa mazao. Mwanachama wa Ushirika Afya atachangia Shilingi 76,800 kwa mwaka na atapatiwa kadi ya bima ya afya ambayo ataitumia kupata matibabu katika vituo zaidi ya 7000 vilivyosajiliwa na Mfuko nchi nzima. Aidha, kupitia utaratibu huu mkulima ana fursa ya kumwandikisha mwenza wake, mzazi au mzazi wa mweza kwa kuongeza malipo ya TZS 76,800 kwa kila mmoja kwa mwaka. Endapo mwanachama wa Ushirika Afya atahitaji kuwasajili watoto katika mpango huu atalipa TZS 50,400 kwa mwaka kwa kila mtoto chini ya miaka 18. Jinsi ya Kujisajili
Ukomo wa Uanachama Kifo; Kukoma kwa uanachama wake katika chama cha msingi; Kushindwa kuchangia michango; na |