Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ikiongozwa na Mwenyekiti Bw. Eliudi Sanga, imefanya ziara ya kikazi mkoani Iringa kwa lengo la kutembelea ofisi za Mfuko na kuzungumza na watumishi.
Wakiwa mkoani humo, walikutana na kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Elius Luvanda, ambapo walijadili kwa kina namna bora ya kuboresha huduma za bima ya afya.
Akizungumza katika kikao cha watumishi wa Mfuko wa Ofisi ya Iringa Bw. Sanga aliwataka kufanya kazi kwa uwajibikaji na bidi ili kuepuka vitendo vya udanganyifu.
Viongozi wengine wa Bodi, akiwemo Dkt. Zubeda Chande na Dkt. George Ruhago, walisisitiza uadilifu kazini, utunzaji wa rasilimali na kuongeza ufanisi wa kazi, hususani katika uchakataji wa madai ya watoa huduma.
Naye mkurugenzi mkuu wa NHIF dkt. Irene Isaka aliwahimiza watumishi kuongeza bidii ili kufanisha lengo la serikali na sera ya bima ya Afya kwa Wote inayotarajia kuanza utekelezaji.
"Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge sasa."*