Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Bw. Eliudi Sanga pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Dkt. Irene Isaka, wamefanya ziara mkoani Iringa pamoja na mambo mengine wamejionea na kupata taarifa ya mradi wa maboresho ya mifumo ya TEHAMA, unatekelezwa ba timu ya Wataalam mkoani humo.
Katika maelezo yake, Mkurugenzi wa huduma za TEHAMA Bw. Alexander Sanga wakati akiwasilisha taarifa ya uandaaji wa mifumo ya utoaji wa huduma kwa njia ya kidijiti mbele ya Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya NHIF,
alianza kwa kuelezea Mfumo wa. NHIF jihudumie (NHIF Self Services) amesema kuwa mfumo huo unatoa fursa kwa wadau wa ndani na wa nje kuweza kujiandikisha na kuandikisha wanachama kupitia watumishi, wakala na makundi mengine yanayoweza kuruhusiwa.
Aidha mfumo huu unaweza kuruhusu Mfuko kufanya mabadiliko katika Vifurushi na vitita vya Mfuko kuendana na mahitaji ya soko ikiwa ni kuongeza na kupunguza vifurushi vya aina mbalimbali vyenye sifa tofauti.
Bw. Alexander amesema
Mfumo huu pia una sifa ya kuweza kuunganishwa na mifumo ya mawakala, ili waweze kuandikisha wanachama kupitia mifumo yao na hadi sasa, kampuni ya simu ya Vodacom ndio wanakamilisha kuunganisha mifumo yake na ya Mfuko ili kuanza usajili kwa kutumia wakala wake walionea nchi nzima.
Mkurugenzi wa Huduma za TEHAMA akiwasilisha taarifa ya utekelzaji wa ujenzi wa Mfumo wa Usajili wa Wanachama Yaani NHIF Self Services kwa Bodi ya Wakurugenzi walipotembelea kituo cha Iringa katika ziara ya kikazi mkoani humo.
Vilevile Bodi iliarifiwa kwamba mfumo unataoa fursa kwa wananchi kutoa mrejesho wa huduma za Mfuko ikiwa ni pongezi, maoni, malalamiko na kufanyiwa kazi kwa njia ya mfumo kwa urahisi.
Bw Alexander aliendelea kusema kuwa pamoja na mfumo huu pia Mfuko umefanya maboresho kwenye ujenzi wa mfumo wa uchakaji wa madai kwa njia ya mtandao ambapo mpaka kufiki juni 2025 mifumo hii imekamilika kwa awamu ya kwanza na kuanza kutumika na wadau.
Alisema kuwa mfumo umerahisha uchakataji wa madai kwa wakati na kurahisisha ulipaji wa madai kwa watoa huduma kwa wakati kutokana na taratibu zote hufanyika kwenye mfumo ukilinganisha na hapo awali.
Alihitimisha kwa kusema kuwa mifumo ya NHIF imeunganishwa na taasisi nyingine kama RITA, NIDA, TIRA, WCF, PSSSF, NSSSF, ZCSRA, BRELA,eGA, UTUMISHI, Wizara ya Afya (MCT na Facility Registry), kupitia mfumo wa Serikali wa GoveESB, ili kurahisisha ubadilishanaji wa taarifa.
Bodi ilipongeza hatua iliyofikiwa katika mradi huo, na kusisitiza kutekelezwa kwa ufanisi zaidi maeneo yaliyobaki ili mradi ukamilike kwa wakati, na hatimaye kupunguza zaidi gharama za uendeshaji.
"Bima ya afya kwa Wote, Jiunge sasa"