MSISHIRIKI UDANGANYIFU - SANGA

Imewekwa: 26 June, 2025
MSISHIRIKI UDANGANYIFU - SANGA

Na Mwandishi Wetu, Njombe

 

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw. Eliud Sanga amewaonya watumishi kutoshiriki katika vitendo vya udanganyifu kuwa makossa hayo bodi haitayafumbia macho.

Akizungumza na watumishi wa Ofisi ya NHIF Mkoa wa Njombe akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani humo Juni 25 2025, amewasihi watumishi kutimiza majukumu yao kwa weledi katika kuwahudumia wanachama kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizopo.

“Tumieni taaluma zenu kuwa wabunifu katika kusajili wanachama kwa kusoma mazingira wanayoyaishi wananchi wa mkoa huu ili kuwa na mbinu sahihi (Best Approach) za kuwashawishi wananchi kujiunga na huduma za NHIF,” alisisitiza.

Mwenyekiti wa Bodi ambaye aliongozana na wajumbe wa Bodi ya NHIF na Menejeimenti ya Mfuko, mbali na kuzungumza na watumishi pia walikutana na uongozi wa Mkoa wa Jombe kwa ajili ya kuimarisha mahusiano na kuweka mikakati ya kuwafikia wananchi.

 

"Bima ya afya kwa Wote, jiunge sasa".