TOTO AFYA KADI

Utangulizi

Ni mpango wa Bima ya Afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18 wanaosajiliwa ili kuwawezesha kupata huduma za matibabu katika vituo vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.

Madhumuni ya Kuanzisha Toto Afya Kadi

  • Kuwapa fursa watanzania wote ambao hawajafikiwa na Mfuko kuwasajili watoto wao.
  • Kuwapa fursa wazazi/walezi ambao ni wanachama wa Mfuko kusajili watoto ambao hawakuweza kusajiliwa kwa sababu nafasi za wategemezi za mwanachama zimejaa,
  • Kutoa nafasi kwa watoto ambao hawana uhusiano wa damu na mwanachama mchangiaji kujisajili na kupata huduma kwa kulipiwa na mzazi au mlezi
  • Kutoa fursa kwa wafadhili au wahisani kuwalipia gharama za usajili watoto walio kwenye mazingira magumu na vituo vya kulelea watoto yatima.

Jinsi ya Kujisajili

  • Mzazi/mlezi atajaza Fomu maalum ya usajili na kubandika picha ya mtoto ya pasipoti.
  • Mzazi/mlezi ataambatanisha nakala ya cheti cha kuzaliwa cha mtoto.
  • Mzazi/mlezi atachangia mara moja kwa mwaka kiasi cha 50,400/= kwa mtoto mmoja.
  • Mwanachama ataanza kupata huduma baada ya siku 90 tangu kukamilika kwa taratibu za usajili na malipo. Iwapo atahuisha uanachama wake ndani ya siku 30 baada ya mwaka wake kuisha, hatakuwa na muda wa kusubiri.