NHIF yapokea Tuzo ya shukrani na uwajibikaji

Imewekwa: 11 July, 2025
NHIF yapokea Tuzo ya   shukrani na uwajibikaji

Makama wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amekabidhi Tuzo ya  Shukrani na Uwajibikaji kwa Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa NHIF Bw. Celestine Muganga aliyepokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Dkt. Irene C. Isaka.

Tuzo hiyo imetolewa na Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika (ASSA) kama shukrani na kutambua mchango na uwajibikaji wa NHIF katika maandalizi ya kongamano la  14 la Kimataifa la Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Africa leo Julai 11, 2025.

Kongamani hilo limefanyika jijini Arusha kwa siku mbili kwenye ukumbi wa AICC ambapo washiriki toka zaidi ya nchi 15 barani Afrika walishiriki.

"Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa".