Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, amtembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati wa kufunga Kongamano la 14 la Kimataifa la Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Africa leo Julai 11, 2025.
Mhe. Othman alitoa pongezi kwa NHIF kwa maboresho mbalimbali yaliyofanyika, ikiwemo matumizi ya mifumo katika utoaji wa huduma kwa wadau. Pia alizungumzia ushirikiano wenye manufaa kati ya NHIF na ZHIF, ushirikiano uliowezesha ZHIF kuchota uzoefu mkubwa toka NHIF. ZHIF imeanza vizuri sana kwakuwa ilikuwa na mahala pa kujifunza alisema Mhe. Othman.
ZHIF ni Mfuko wa Bima ya Afya wa Zanzibar ulioanzishwa mwaka 2023.
"Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa".