Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) Tanzania, Dk. Irene C. Isaka, akiwasilisha mada katika Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani leo Julai 10, 2025, jijini Arusha, Tanzania, alielezea nafasi ya NHIF katika kutekeleza Sera ya Bima ya Afya Kwa Wote (UHI), ambayo inakusudia kuwapa Watanzania wote, uwezo wa kupata huduma bora za afya bila kizuizi cha fedha.
Adhima hiyo inayoenda sambamba na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.
Wasilisho hilo pia lilioyesha jukumu la NHIF katika kukuza uchumi wa Tanzania kwa kupunguza gharama za afya zinazolipwa moja kwa moja na watu, na hivyo kuwezesha jamii kuwekeza katika maeneo mengine muhimu, na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa. Kauli za Dk. Isaka katika mkutano huo zilitia mkazo msimamo wa NHIF wa kusaidia mabadiliko ya mfumo wa afya nchini Tanzania kupitia utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya Kwa Wote na mikakati endelevu ya ufadhili wa sekta ya afya.
"Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa".