Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani NHIF Yaandaa Iftar Maalum ya Mfungo Ranadhan na Kwaresma

Imewekwa: 02 March, 2026
Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani NHIF Yaandaa Iftar Maalum ya Mfungo Ranadhan na Kwaresma

28.01.2026  Dodoma

Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, uliandaa Iftar maalum kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na Kwaresma. Futari hiyo iliandaliwa kwa ajili ya watumushi wanawake toka ofisi za Mfuki nchi nzima, watumishi wa makao makuu, watumishi wa ofisi ya mkoa wa Dodoma pamoja na wadau mbalimbalu wa Mfuko.

Katika Iftar hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dkt. Irene Isaka awapongeza watumishi wa Mfuko (NHIF) kwa utendaji kazi wao mzuri na kujituma katika kuwahudumia wananchi.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa futari hiyo alisema anajivunia mshikamano, nidhamu na weledi unaooneshwa na timu ya watumishi katika kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora na kwa wakati.

Futari hiyo iliwakutanisha watumishi pamoja na wageni mbalimbali, wakiwemo Waislamu wanaotekeleza ibada ya Ramadhani na Wakristo wanaoendelea na mfungo wa Kwaresma, ikiwa ni ishara ya umoja, upendo na kuheshimiana miongoni mwao.

Aidha, aliwahimiza watumishi kuendelea kuonyeshana upendo, mshikamano na kuvumiliana hasa katika kipindi hiki cha mfungo, huku akisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na uwajibikaji ili kuikuza taasisi na kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wanachama nchini.

Bima ta Afya kwa Wote, Jiunge Sasa