NHIF na ZHSF zaingia makubaliano ya kihuduma

NHIF na ZHSF zaingia makubaliano ya kihuduma Jul 19, 2024

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Bernard Konga na Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar ( ZHSF) ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Yaasin Juma wameingia Mkataba wa makubaliano wa utoaji huduma za matibabu kwa wanachama wa ZHSF kupitia vituo vilivyosajiliwa na NHIF Tanzania Bara kuanzia Julai Mosi, 2024.

Hatua hii ni muhimu katika utekelezaji wa maamuzi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu wanapozihitaji bila kikwazo chochote.

ZHSF wameishukuru NHIF kwa mchango mkubwa ilioutoa katika mchakato mzima wa uanzishaji wa Mfuko huo na kuahidi ushirikiano katika utekelezaji wa mkataba huo.

Bw. Konga amewahakikishia wanachama wa ZHSF kuwa Mfuko umejipanga kutekeleza majukumu kwa mujibu wa makubaliano yaliyoingiwa ili kuhakikisha wanachama wa pande zote mbili wanapata huduma stahiki na bora.