Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ni miongoni mwa Taasisi zilizokabidhiwa Cheti cha Uwekezaji katika Amana ya SUKUK ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Cheti hicho kilikabidhiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein ali Mwinyi katika hafla iliyofanyika Ikulu Zanzibar Aprili 29,2025 ambapo NHIF iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Bw. Celestine Muganga kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Dkt. Irene Isaka.
Hatua hiyo ni kuthibitisha kuwa Mfuko utafanya uwekezaji kwenye SUKUK ambao umezingatia misingi ya Sheria na una manufaa kwa Mfuko na kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hususan katika kuleta maendeleo ya wananchi.
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa