WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungani Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameridhishwa na namna Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ulivyojipanga kutekeleza Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.
Waziri Mkuu, ameyasema hayo Oktoba 10, 2025 jijini Mbeya alipotembelea banda la NHIF kwenye maadhimisho ya wiki ya vijana inayofanyika mkoani humo.
Amesema Sekta ya afya ni eneo muhimu na ndiyo maana Serikali imeweka bima ya afya kwa wote ili watu wapate matibabu ya uhakika.
"Hivyo ni vyema mkaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya ili wawe na uhakika wa matibabu pale watakapo ugua.
Ameagiza Mfuko kuyafikia makundi mbalimbali hasa vijana wakiwemo: Wakulima, Wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo, madereva wa mabasi na malori, waendesha bodaboda, bajaji , wajasiriamali na wananchi kwa ujumla ili wajiunge na NHIF" alisisitiza Mh.Waziri Mkuu.
Awali Meneja wa NHIF mkoa wa Mbeya Dkt. Eliud Kilimba alimweleza Waziri Mkuu kwamba namna NHIF ilivyojipanga kutekeleza Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, jitihada zitakazowezesha Watanzania wote kuwa na uhakika wa matibabu.
Aidha Dkt. Kilimba alisema NHIF inashiriki kwenye maonesho hayo kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu kwa vijana na wananchi kwa ujumla ili wajiunge na Mfuko kupitia vitita mbalimbali vilivyoanzishwa na Mfuko.
Pia kupitia maonesho haya tunatoa elimu kwa wananchi na wadau kuhusu maboresho yaliyofanyika upande wa mifumo ili kurahisisha huduma, alisema Dkt. Kilimba.
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa