Dodoma, Tanzania – Julai 21, 2025
Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Risk champions wamepatiwa mafunzo maalum ya udhibiti wa majanga kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa ISO - 9001:2015 na Mfumo wa COSO (COSO framework). Mafunzo haya yanalenga kuwaongezea uelewa na uwezo wa kushughulikia changamoto mbalimbali zinazoweza kuathiri utendaji wa Mfuko.
Mafunzo hayo yameandaliwa mahsusi kwa maofisa wanaowakilisha vitengo mbalimbali pamoja na Ofisi za NHIF za Mikoa.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, *Dkt. Irene Isaka*, alieleza kuridhishwa kwake na namna watumishi wanavyojifunza mbinu mbalimbali za kudhibiti majanga katika maeneo yao ya kazi. Alisisitiza kufanyakazi kwa kuzingatia maadili na Sheria kanuni na taratibu. Kwani alisema kama tutazingatia na kuishi kwenye maadili yetu ya msingi tutaikinga taasisi yetu na majanga. Alieleza kwa undani umuhimu wa Uadilifu, uwajibikaji, ubunifu, heshima, haraka na hadhari.
Pia alisema kuwa mafunzo haya ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa mkakati wa Mfuko na kuulinda dhidi ya athari za majanga mbalimbali.
“Mafunzo haya ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa NHIF inakuwa na mifumo madhubuti ya kudhibiti majanga. Tutahakikisha kuwa mafunzo haya yanakuwa endelevu ili kuimarisha utayari wa watumishi wetu,” alisema Dkt. Isaka.
Mafunzo hayo yanayofanyika jijini *Dodoma* yameanza tarehe *14 Julai* na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe *23 Julai 2025, yakihusisha jumla ya **washiriki 47* kutoka vitengo mbalimbali vya NHIF.
Wakufunzi wa mafunzo hayo, *Bw. Felix Kapesula* na *Bw. Peter Mbelwa, ambao ni wataalamu kutoka nje ya Taasisi, walisisitiza umuhimu wa kuwajengea uwezo Menejimenti ya Mfuko. Aidha, walipongeza NHIF kwa kuwa na **kitengo maalum cha udhibiti wa majanga*, wakisema ni hatua muhimu ya kimkakati katika taasisi yoyote inayojali uimara wake.
Bima ya afya kwa wote, Jiunge sasa