Watumishi NHIF ZINGATIENI MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA - Dkt.ISAKA

Imewekwa: 09 July, 2025
Watumishi NHIF ZINGATIENI MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA - Dkt.ISAKA

Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Kilimanjaro,wameaswaa kuzingatia kanuni na taratibu za utumishi wa umma katika maeneo yao ya kazi, hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt.Irene Isaka akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro.

Dkt. Isaka alifika katika Ofisi za NHIF Mkoani hapa kwa lengo la kuona namna watumishi wanavyotoa huduma lakini pia kuzungumza nao ili kupata maoni na changamoto zao.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu aliwaeleza Watumishi hatua mbalimbali zinazofanyika katika uboreshaji wa maslahi ya watumishi katika eneo la kazi.

Kwa upande wao Watumishi wamempokea Mkurugenzi  kwa furaha kubwa na kupongeza Mfuko kuboresha mazingira ya kazi kwa kuwawezesha kuhamia katika ofisi mpya kubwa na yenye nafasi  ambayo inawawezesha kufanya kazi katika mazingira mazuri na kutoa huduma bora kwa wanachama.

Aidha waliomba Mfuko kuenedelea kuwawezesha katika fursa za mafunzo ya mara kwa mara ili kuzifahamu fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi. 

*"Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa".