OFISI YA WAZIRI MKUU YAGHARAMIA BIMA YA AFYA YA NHIF KWA WANACHUO VETA - KARAGWE
OFISI YA WAZIRI MKUU YAGHARAMIA BIMA YA AFYA YA NHIF KWA WANACHUO VETA - KARAGWE
Imewekwa: 24 June, 2026
Kagera, 25 Juni 2026
Ofisi ya waziri Mkuu inatekeleza bima ya Afya kwa wote kwa kufadhili vijana 125 walio kwenye mazingira magumu ambao wepewa ufadhili wa OWM kwenye chuo cha VETA Karagwe.
Akizungumza kwenye ghafla ya ugawaji wa kadi. Mkurugenzi Mkuu wa NHIF aliishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kugharamia bima ya Afya kwa wanafunzi hao. Aliwahamasisha vijana hao kuwa mabalozi wa Bima ya Afya kwa vijana wenzao.
Ofisi ya NHIF Karagwe imefanikiwa kukifikia Chuo cha VETA Karagwe ambapo imesajili wana chuo 125 na kukabidhi kadi 69 za matibabu kwa wanafunzi chuoni hapo.
Katika hafla hiyo ya ugawaji wa kadi hizo ambayo iliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene Isaka ambaye aliishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kugharamia bima ya afya kwa wanafunzi hao, jambo ambalo linaonesha dhamira ya Serikali katika kuboresha ustawi na maendeleo ya vijana kupitia upatikanaji wa huduma za afya.
“Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utaendelea kushirikiana kwa karibu na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na taasisi zingine ili kuhakikisha makundi mbalimbali ya wananchi yanapata ulinzi wa afya kupitia bima ya afya,” alisema Dkt. Isaka.
Katika kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi za hifadhi ya jamii, Dkt. Isaka aliambatana na maafisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wa Wilaya ya Karagwe, ambao walishiriki katika utoaji wa elimu na ugawaji wa kadi kwa wanafunzi hao.
Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za NHIF za kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa bima ya afya na utekelezaji wa dira ya Serikali ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za afya kwa uhakika.
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa