Katika Maonesho ya 12 ya Biashara na Utalii yaliyoandaliwa na TCCIA-Tanga kuanzia Mei 26 hadi Juni 9, 2025, Ofisi ya NHIF Mkoa wa Tanga imeibuka Mshindi wa Kwanza kwenye kundi la Taasisi za Huduma za Bima ya Afya na Pensheni
Ofisi hiyo ilitumia jukwaa hilo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali za bima ya afya, ikiwemo vifurushi vipya kama Toto Afya, pamoja na kufanya ziara kwa waajiri na washiriki wa maonesho hayo ili kuhamasisha matumizi NHIF juhudumie (Self Service).
Ushiriki wao umeonesha dhamira ya dhati katika kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwahamasisha kujiunga na Bima ya Afya ili wawe na uhakika wa matibabu.
Katika picha ni watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga wakitoa elimu kwa wananchi ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko katika maonesho ya 12 ya utalii yaliyoafanyika jijini Tanga kuanzia tarehe 26 mei hadi 09 June 2025