Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanikiwa kutoa elimu kuhusu bima ya afya kwa wote katika Kongamano la Sayansi ya Masuala ya Afya lililofanyika katika mji wa Serikali Mtumba, Dodoma. Tukio hilo lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) limewakutanisha wataalamu wa afya kutoka ndani na nje ya nchi, wakiwemo Maprofesa kutoka vyuo maarufu kama Harvard.
Kupitia banda lao la maonyesho, NHIF iliwaelimisha washiriki kuhusu umuhimu wa bima ya afya, upatikanaji wake kwa wote wakiwemo wasiokuwa na ajira rasmi, na mchango wake katika kuboresha huduma za afya nchini.
Meneja Uhusiano wa NHIF, Bw. James Mlowe na timu ya viongozi wa masoko na wa ofisi ya NHIF mkoa wa Dodoma, walieleza kuwa ushiriki huo ni sehemu ya juhudi za mfuko huo kuhakikisha kila Mtanzania anaelewa haki na faida za kuwa na bima ya afya.
Washiriki walionesha kuvutiwa na juhudi hizo, huku baadhi wakipendekeza ushirikiano wa utafiti na kubadilishana uzoefu kati ya NHIF na taasisi zao.
Wananchi waliotembelea banda la NHIF wakijihudumia kwa kutumia Mfumo wa NHIF Self Service kwa kutumia simu zao.