Yang'ara kwenye utunzaji wa mazingira
Kagera, 22 April 2026.
0fisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Kagera, imeungana na uongozi na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Buhembe katika zoezi la upandaji miti, zoezi lililofanyika shuleni hapo tarehe 22 Aprili 2026.
Zoezi hilo, linaendelea kutambulisha dhamira ya dhati ya NHIF katika jitihada za utunzaji wa mazingira, jitihada zinazolenga kupunguza hewa ukaa ili kupambana na ongezeko la joto duniani.
Baada ya kuhitimishwa kwa zoezi hilo, Meneja wa NHIF mkoa wa Kagera Bw. Ismail Kangeta aliwasihi wanafunzi wa shule hiyo kuwa marafiki wa mazingira kwa kuendelea kupanda miti na kutunza iliyopandwa ili ikue na kutimiza malengo tarajiwa. Aidha Bw. Kangeta alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wanafunzi kujiunga na bima ya afya kupitia kifurushi cha wanafunzi kinachogharimu TZS. 50,400 tu kwa mwaka, ili kujihakikishia huduma za matibabu wakati wowote wanapougua.
Zoezi hili ni mwendelezo wa zoezi lililozinduliwa rasmi na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Dkt. Irene Isaka, uzinduzi uliofanyika tarehe 08 Aprili 2026, siku ya Wanawake Duniani, ambapo Dkt. Isaka aliongoza watumishi wanawake wa Mfuko kupanda miti mkoani Dodoma katika ofisi za makao makuu ya NHIF, mji wa serikali Mtumba na hospitali ya Uhuru iliyopo Chamwino. Utunzaji wa mazingira itaendekea kuwa agenda ya kudumu ya Mfuko ili kuunga mkono jitihada za kitaifa na kimataifa za utunzaji wa mazingira, alisema Dkt. Isaka wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo.
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa