Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeshiriki katika ufunguzi rasmi wa Michezo ya Mei Mosi, michezo inayofanyika mjini Njombe, hafla ya ufunguzi imewakutanisha watumishi kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi kwa lengo la kuimarisha afya, mshikamano na tija mahali pa kazi.
Watumishi wa NHIF walijitokeza kwa wingi kushiriki katika michezo mbalimbali, wakionesha ari, nidhamu na mshikamano unaoakisi dhamira ya Mfuko katika kuhamasisha maisha yenye afya kwa watumishi.
Akizindua mashindano hayo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo aliwapongeza viongozi wa taasisi zote zilizopeleka timu kushiriki michezo ya Mei Mosi. Alisema hatua hiyo ni muhimu katika kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha watumishi wanakuwa na afya njema, jambo litakalowawezesha kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuchangia kikamilifu katika ujenzi wa taifa.
NHIF imeendelea kusisitiza umuhimu wa michezo na mazoezi kama sehemu ya kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza (NCDs), huku ikihamasisha watumishi na wananchi kwa ujumla kujenga utamaduni wa kujali afya zao.
Ushiriki wa NHIF katika Michezo ya Mei Mosi ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya Menejimenti ya Mfuko chini ya Mkurugenzi Mkuu Dkt. Irene C. Isaka katika kuendeleza ustawi wa watumishi na lengi mahsusi la Mfuko kuwa mfano bira kwa jamii katika kuhamasisha mtindo bora wa maisha.
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!