Dodoma 29/04/2026
Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), chini ya Mwenyekiti wake Bw. Eliud Sanga, imekutana jijini Dodoma kwa lengo la kupokea taarifa ya maendeleo ya Mfuko kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/26.
_1777881881.jpeg)
Kikao hicho kimefanyika tarehe 29 Aprili, 2026 kikitanguliwa na vikao vya kamati za Bodi vilivyofanyika tarehe 27 - 28 April, 2026. Kamati hizo ni Kamati ya Fedha na Uendeshaji (Finance & Operations Committee) chini ya Mwenyekiti Prof. George Ruhago, Kamati ya Ukaguzi na Hadhari ya Vihatarishi (Audit & Risk Commitee) chini ya Mwenyekiti CPA. Veronica Kishala na Kamati ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala Bora ( Human Resources and Governance Committee) chini ya Kaimu Mwenyekiti Wakili. Shaaban Kabunga.
Wajumbe wengine wa Bodi waliohudhuria kikao hicho ni Prof. Ramaiya Kaushik na Bi. Zubeda Chande.
Wenyeviti wa Kamati mara baada ya kuwasilisha taarifa zao mbele ya Bodi, Mwenyekiti wa Bodi pamoja na Wajumbe wengine kwa pamoja waliipongeza Menejimenti ya Mfuko kwa mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha robo ya tatu.
Bodi ilipongeza mafanikio ya usajili wa wanachama yaliyofikia asilimia 58, aidha kuendelea kupungua kwa siku za ulipaji madai kwa watoa huduma (aging), kadhalika Bodi ilipongeza ( investment performance, vilevile Bodi iliendelea kupongeza matokeo mazuri kwenye ukuaji wa rasilimali za Mfuko pamoja na ziada (surplus) inayoendelea kukua zaidi.
Vilevile walipongeza mazoezi kwa watumishi na ushiriki wao kwenye michezo ya Mei Mosi pamoja na marathon ambazo zaidi ya watumishi 168 wamekuwa wakishiriki
Pamoja na pongezi hizo Bodi ilitoa maelekezo kadhaa ili kuboresha za kulinda mafanikio yaliyopatikana;

i. Mfuko uendelee kufanya uwekezaji makini ili kuongeza ukwasi kwa ajili ya kujenga uwezo zaidi wa kifedha na kutengeneza ziada kubwa zaidi;
ii. Kuendelea kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima na kupambana zaidi na vitendo vya udanganyifu,
iii. Bodi ilielekeza kuendelea kutoa elimu kwa watoa huduma kuhusu fursa ya mikopo ya NHIF ili wafunge vifaa vya utambuzi wa wanachama kupitia alama za vidole (biometric verification).
iv. NHIF tuendelee kuwa mfano wa kuigwa katika jitihada za kupambana na magongwa nyemelezi (NCDs) ili jamii na hatimaye kuepukana na gharama kubwa za kutibia magonjwa hayo;
v. Kuendelea kutekeleza ESG kwa kupanda miti na kupunguza matumizi ya karatasi
vi. Mfuko uendelee na hatua mbalimbali za kutatua changamoto za watumishi kupitia njia mbalimbali ikiwemo HR Clinics.
vii. kwa upande mwingine Bodi ilielekeza watumishi nao kutimiza wajibu wao pamoja na kufuata Sheria, miongozo na taratibu katika kutekeleza majukumu yao;
viii. Menejimenti iendelee kufanyia kazi hoja wa wakaguzi wa ndani na ukaguzi wa nje. Vilevile kutekeleza kwa wakati mapendekezo ya Wadhibiti pamoja na Actuarial recommendations.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Dkt. Irene Isaka aliishukuru Bodi kwa kuendesha kikao vizuri pamoja na miongozo mbalimbali inayotolewa na Bodi, kwani miongozo hiyo imekuwa chachu kubwa ya kuteleleza majukumu ya Mfuko kwa mafanikio. Aidha aliihakikishia Bodi kuwa Menejimenti inafanyia kazi maelekezo yote ya Bodi ili kuboresha zaidi ustawi wa Mfuko.
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa