NHIF, UBALOZI WA RWANDA WAJADILI BIMA YA AFYA

Imewekwa: 13 August, 2025
NHIF, UBALOZI WA RWANDA WAJADILI BIMA YA AFYA

NHIF, UBALOZI WA RWANDA WAJADILI BIMA YA AFYA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa Kinondoni imekutana na Ofisi ya Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania kujadili upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watumishi wa Ubalozi na wategemezi wao.

Kikao kimeongozwa na Balozi wa Pili, Bi. Epiphania Buzizi ambaye ameridhia watumishi wote pamoja na familia zao kuanza kupata huduma za ziada kuanzia *Septemba 2025*.

Mhe. Balozi amepongeza uongozi wa NHIF kwa maboresho yanayoendelea kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma bora za bima ya afya.

Kwa upande wa Meneja wa NHIF Mkoa wa Kinondoni Dkt. Raphael Mallaba umemhakikishia Mhe. Balozi huduma bora kwa Watumishi wa Ubalozi na Familia zao, aidha Dkt. Mallaba alielezea maboresho mbalimbali yaliyofanyika kwenye Mfuko kwa lengo la kuboresha huduma, jambo lililovutia kwa kiasi.kikubwa Maofisa Ubalozi.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!