WATUMISHI WA NHIF WAFIKISHA BENDERA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

Imewekwa: 15 January, 2025
WATUMISHI WA NHIF WAFIKISHA BENDERA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya walishiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro la “Twenzetu Kileleni” lililoratibuwa na Shirika la Hifadhi za Taifa kwa lengo la kupaisha bendera ya Bima ya Afya kwa Wote katika Kilele cha Mlima huo.

Watumishi wawili (2) kutoka NHIF ambao ni Raymond Massai na Twahiru Hauke walifanikiwa kufika kileleni baada ya safari ya siku takriban 6 zilizojawa na hekaheka za kupanda mlima huo.

Watumishi hao wa NHIF walitumia fursa hiyo kutoa elimu ya Bima ya Afya na huduma za NHIF kwa washiriki katika zoezi hilo ili kuendelea kujenga uelewa wa huduma za bima ya afya miongoni mwa wanachama na wasio wanachama. Wanachama waliopewa elimu hiyo ni pamoja na watumishi wa TANAPA na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wasio wanachama ni pamoja na wapagazi walioshiriki zoezi hilo.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!