Watumishi 48 wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wameshiriki mbio kimataifa za Kili marathon zilizofanyika mkoani Kilimanjaro tarehe 22 Machi, 2026. Watumishi walishiriki mbio za KILOMETA 42, KILOMETA 21 na KILOMETA 5 wakiungana na washiriki maelfu toka nchini na nchi za nje.
Ushiriki huo ni mwendelezo wa juhudi za uongozi wa Mfuko kuhamasisha watumishi kuwa mfano kwa jamii katika ushiriki wa mazoezi kwa kutoa hamasa kwa jamii kuzingatia afya kupitia mazoezi, ikizingatiwa kuwa watumishi wengi wa maofisini hukaa muda mrefu kila siku wakati wa kutekeleza majukumu yao, hali inayochangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa nyemelezi ( Non- Communicable Diseases).
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene C. Isaka, ameendelea kuwa kinara wa kuhamasisha utamaduni wa kufanya mazoezi kwa watumishi, akisisitiza umuhimu wa kuwa na afya njema kwa ustawi binafsi na ufanisi kazini.
Mfuko utaendelea kudhamini watumishi wanakaoonesha nia ya kushiriki mazoezi mbalimbali kwa lengo la kuwa na nguvu kazi imara kwa tija ya Mfuko, alisema Dkt. Isaka.
Kati ya washiriki 48 walioshiriki mbio hizo, watumishi 41 walikimbia umbali wa kilomita 42, huku wengine wakishiriki mbio za kilomita 21 na kilometa 5.
NHIF inaendelea kuweka michezo kuwa kipaumbele, sambamba na kuunga mkono sera za kitaifa na kimataifa zinazolenga kujenga jamii yenye watu wenye afya bora.
Bima ta Afya kwa Wote, Jiunge Sasa
#NHIF #AfyaKwanza #PambanaNaMagonjwaYasiyoambukiza #FanyaMazoezi