NHIF NA TCB WAJADILI UTEKELEZAJI WA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Imewekwa: 12 June, 2025
NHIF NA TCB WAJADILI UTEKELEZAJI WA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dkt. Irene C. Isaka amefanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB Bw. Adam Mihayo. Mazungumzo hayo yalilenga kuangalia jitihada za pamoja baina ya NHIF na Benki hiyo katika utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote. 

Kikao hicho kimefanyika tarehe 6 Juni, 2025 katika Ofisi za Makao Makuu ya NHIF Jijini Dodoma. 

Katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB aliambatana na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa TCB Bw. Richard Mtapa na Meneja wa Huduma za Biashara ya Serikali Bw. Sepi Mawalla.

Katika picha katikati ni Mkurugenzi Mku wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dkt. Irene Isaka akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa benki ya TCB walipofanya majadiliano ya namna ya utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote.