Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekutana na kufanya mazungumzo na Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI), mazungumzo yaliyofanyika jijini Dodoma.
Mazungumzo hayo yaliongozwa na Mkurugenzi wa Tiba na Huduma za Kitaalam Dkt. David Mwenesano kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Dkt. Irene C. Isaka, kwa upande wa MOI timu iliongozwa na Dkt. Laurent Mchome.
Mazungumzo hayo yalilenga katika kuimarisha ushirikiano utakaowezesha kuboresha zaidi huduma kwa wanachama wa Mfuko wanaopata huduma kupitia Taasisi ya MOI.
Katika majadiliano hayo, Taasisi zote mbili zimekubaliana kuwa na mawasiliano wakati wote ili linapotokea jambo linalohitaji maamuzi ya pamoja linatafutiwa suluhu kwa haraka.
"Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa".