Dodoma, 14 Julai 2025
Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Irene C. Isaka imekutana na wawakilishi wa kampuni ya Gentell ya nchini Uingereza wakiingozwa na Dkt. Rupinder Singh na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuboresha huduma kwa wanachama wa Mfuko.
Awali Mwakilishi wa kampuni ya Gentell Dkt. Singh alieleza kuwa kampuni yao imebobea katika kutoa huduma za tiba ya majeraha na vidonda, ikiwemo utengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa hayo.
Katika mazunvymzo yake Dkt. Singh alionesha nia ya kampuni yao kujenga kiwanda cha vifaa tiba hapo nchini, hali ikayosaidia kupungua kwa gharama za matibabu ya wagonjwa wa majeraha na vidonda pamoja na kutoa ajira kwa watanzania.
Aidha Mwakilishi huyo alielezea nia ya kampuni yao kufungua Kliniki za kibingwa hapa nchini maalum kwa kutoa huduma kwa wagonjwa wa majeraha na vidonda, kwa kutumia mbinu za kisasa zinazopelekea majeraha kupona kwa haraka, hali itakasaidia kupungua kwa gharama za NHIF.
Picha ya pamoja ya menejimenti ya Mfuko wakiwa pamoja wadau kutoka Gentell walipomtembelea Mkurugenzi Mkuu ofisini kwake mapema wiki hii.
Kwa upande wa NHIF, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Dkt. Isaka, alielezea namna NHIF inavyofanya kazi, na hivyo kuwakaribisha Gentell kwenye soko la huduma, pindi watakapokamilisha taratibu za kufungua Kliniki zao na kupata ithibati toka mamlaka zinazohusika.
Mazungumzo hayo yalishuhudiwa na Wawakilishi toka Wizara ya Afya wakiongozwa na Dkt. Timothy Wonanji.
Pande zote mbili zilihitimisha mazungumzo hayo, kwa kukubaliana kuendeleza mawasiliano na ushirikiano ili kufikia adhima ya masuala yote yaliyojadiliwa.
"BIMA YA AFYA KWA WOTE, JIUNGE SASA".