NHIF/MUHAS KUSHIRIKIANA KIMKAKATI KWENYE UTEKELEZAJI WA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Imewekwa: 22 May, 2026
NHIF/MUHAS KUSHIRIKIANA KIMKAKATI KWENYE UTEKELEZAJI WA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeingia makubaliano ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), hatua inayolenga kuimarisha tafiti, ubunifu na ufanisi katika utoaji wa huduma za bima ya afya nchini.

Makubaliano hayo yamesainiwa  Mei 20, 2026 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Dkt. Irene Isaka pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Prof. Apolinary Kamuhabwa.

Akizungumza baada ya hafla ya utiaji saini, Dkt. Isaka alisema ushirikiano huo ni hatua muhimu ya kuendelea kuboresha huduma zinazotolewa na Mfuko kwa wanachama na wananchi kwa ujumla hasa kwa wakati huu ambapo utekekezaji wa Sheria ya Bima ya Afys kwa Wote ukiwa unaendelea.

Alisema kupitia makubaliano hayo, taasisi hizo mbili zitashirikiana kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za NHIF, hususan katika maeneo ya mifumo ya utoaji huduma, matumizi ya teknolojia, tafiti za afya pamoja na uchambuzi wa sera na mwenendo wa huduma za bima ya afya.

“Ushirikiano huu utasaidia kupata tafiti na takwimu sahihi zitakazowezesha kufanya maamuzi yenye tija kwa maendeleo ya sekta ya afya na kuboresha huduma kwa wanachama wetu hasa kipindi hiki tunapotarajia ongezeko kubwa la wananchi kupata matibabu kipitia utaratibu wa bima,” alisema Dkt. Isaka.

Kwa upande wake, Prof. Kamuhabwa alisema MUHAS ipo tayari kutumia utaalamu wa watafiti na wabobezi wake kushirikiana na NHIF katika tafiti zitakazochangia maendeleo ya sekta ya afya nchini.

Alieleza kuwa makubaliano hayo yatafungua fursa zaidi za ubunifu, mafunzo na tafiti zitakazosaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya pamoja na kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi.

Bima ya Afys kwa Wote, Jiunge Sasa

slot gacor