Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dkt. Irene C. Isaka amekutana na Watumishi wa NHIF Mkoa wa Manyara tarehe 09 Julai, 2025 ambapo amewahimiza kufanya kazi kwa bidii, kwa kuwafikia wananchi wengi na kuwasajili ili wapate huduma za bima ya afya.
Mkurugenzi Mkuu amesisitiza umuhimu wa watumishi wa Mfuko kutoa huduma kwa weledi na ubora kwa Wadau ili kuondoa malalamiko yanayochafua taswira ya Mfuko.
pamoja na hayo Dkt.Isaka alitumia fursa hiyo kuzunguza na watumishi kuhusu jitihada mbalimbali zinazofanyika kwa ajili ya kuboresha ustawi wao.
Kwa Upande wa Watumishi wameonesha kufurahishwa kwa kupatiwa vitendea kazi ambavyo vinawarahisishia katika utoaji wa huduma ikiwemo usajili wa wananchi katika huduma za bima.
Aidha watumishi hao wameomba menejimenti ya Mfuko kuandaa Fao la ushirika kwa ajili ya wakulima kwani hapo awali mapokeo yake kwa wakulima yalikuwa ni mazuri sana.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa kuzifikia Ofisi zote za NHIF ili kuona utendaji kazi, huduma kwa wadau na kusikiliza mawazo, maoni na changamoto za Watumishi.
"Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa'.