30 Julai, 2025-Dodoma
Mkurugenzi Mkuu Dkt. Irene C. Isaka leo tarehe 30 Julai, 2025 amekutana na Maofisa Wateule watakaokuwa Viongozi wa ofisi mpya nane zinazofunguliwa na Mfuko kwa ajili ya kuboresha huduma kwa Wanachama na Wadau.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya Mfuko, Dkt. Isaka alisema, utelelezaji wa Bima ya Afya kwa wote tunahitaji kuwa karibu zaidi na wanachama. Ofisi hizo za kimkakati pamoja na kusogeza huduma kwa Wanachama pia zinalenga kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya Mfuko, ikiwemo usajili wa Wanachama wapya kutoka makundi mbalimbali. Mwaka wa fedha 2025/26 tumeweka malengo ya kusajili wananchi zaidi ya milioni 1.9.
Ofisi hizo mpya zinafunguliwa maeneo ya Ifakara mkoani Morogoro, Masasi mkoani Mtwara, Karagwe mkoani Kagera, Kahama mkoani Shinyanga, Tegeta mkoani Dar es Salaam, Bukombe mkoani Geita, Nzega mkoani Tabora na Mbinga mkoani Ruvuma.
Katika picha ni Wasimamzi viongozi wa Ofisi nane za Mfuko zilizoanzishwa katika wilaya ili kusogeza huduma karibu na wananchi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu Dkt.Irene C.Isaka aliyekaa katikati, akiwa pamoja na Mkurugenzi wa huduma za Uanachama Dkt.Alphonce Chandika, na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw.Lembris Laanyuni mara baada ya kikao cha kukabidhiwa majukumu.
Katika kikao hicho Mkurugenzu Mkuu, aliwapongeza Viongozi hao na kuwapa moyo wa kwenda kutekeleza majukumu yao kwakuwa Bodi na Menejimenti ya Mfuko imewaamini kutokana na historia yao ya uchapa kazi pamoja na sifa za uongozi walizonazo.
Kwa upande wa Viongozi hao wapya, walishukuru kwa Menejimenti kuonesha imani kwao, na wameahidi kwenda kutekeleza majukumu yao mapya kwa uwezo wao wote na hatimaye kufikia malengo ya Mfuko.
Kikao hicho kilihudhuliwa na Wajumbe wa Menejimenti ambao pia walipata fursa ya kutoa nasaha kwa Viongozi hao wapya. Wajumbe wa Menejimenti walisisitiza ubunifu, kuimarisha mahusiano na wadau, kujifunza tamaduni na desturi za naeneo wanayohudumia, kutoa huduma bora kwa wadau na kuheshimu misingi ya utendaji kazi ya Mfuko.
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa