Leo tarehe 21.06.2025 Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umepokea Tuzo Maalum kutoka kwa Chama Cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam (DPC), Tuzo hiyo imejielekeza kuipongeza Taasisi ya NHIF kwa Kazi kubwa ambayo inafanya katika kuhudumia Watanzania na Ushirikiano Mkubwa ambao unaendelea kuutoa kwa Waandishi wa Habari wakati wote.
Akipokea Tuzo hiyo kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Ofisi ya Mkoa wa Temeke Bw. Cannon Luvinga amesema "Tunashukuru kwa Tuzo hii kutoka kwenu Waandishi wa Habari na sisi kama Taasisi tuna Wajibu Mkubwa wa Kuendelea kuelimisha Wananchi kuhusiana na Umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Ili waweze kuwa na Uhakika wa Matibabu nyakati zote. Lakini kazi hii ya Uelimishaji Wananchi inategemea sana Mashirikiano na Waandishi wa Habari Ili kuhakikisha Elimu inafika kwa Wananchi kwa Ukubwa wake"
Zaidi Ndugu Luvinga alitoa Elimu ya Huduma zote ambazo Mfuko unazitoa kwa Wanachama wake na alitumia Jukwaa Hilo kuwaelimisha Waandishi wa Habari kuhusu BIMA YA AFYA KWA WOTE na jinsi Taasisi ya NHIF ilivyojipanga kutekeleza hili Ili kuhakikisha kila Mtanzania anajiunga na Bima ya Afya kama ambavyo Maelekezo ya Mh. Rais ya kutaka kila Mtanzania kujiunga na Bima ya Afya.
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wa Chama cha Waandhishi wa Habari jijini Dar es Salaam uliofanyika tarehe 12 Mei, 2025
Vile vile aliwaasa Waandishi wa Habari kujiunga na Mfuko huo na ametoa Ahadi ya kukutana na Viongozi wa Waandishi wa Habari kwaajili ya Kuanza Mchakato wa kuwasajili Waandishi wote wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam bila kumuacha Mwandishi yoyote nyuma.
Tuzo hiyo imetolewa leo katika Mkutano Mkuu wa Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo.