Makamu wa Rais Dkt. Mpango Asisitiza Bima ya Afya Kwa Wote

Imewekwa: 10 July, 2025
Makamu wa Rais Dkt. Mpango Asisitiza Bima ya Afya Kwa Wote

Makamu wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philipo Mpango atembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Barani Africa leo Julai 10 mwaka 2025, jijini Arusha na kusisitiza umuhimu wa kila Mtanzania kuwa na bima ya afya.

"Hakuna njia nyingine, kila Mtanzania lazima awe na bima." Alisema Mhe. Mpango.

Dkt. Mpango alipongeza juhudi zinazofanywa na NHIF za kupanua upatikanaji wa huduma za afya na kusisitiza msimamo wa Serikali katika kufikia Bima ya Afya kwa Wote, akibainisha kuwa bima ya afya si tu kipaumbele cha Serikali, bali ni muhimu kwa usalama wa kifedha kwa wananchi na maendeleo ya Taifa.

"Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa".