Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dkt. Irene C. Isaka amekutana na kufanya mazungumzo na Maofisa wa Jeshi la Magereza toka Makao Makuu, lengo la mazungumzo hayo ni mwendelezo wa mashirikiano baina ya NHIF na Jeshi la Magereza.
Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 6 Juni, 2025 katika Ofisi za Makao Makuu ya NHIF Jijini Dodoma ni Pamoja na Maboresho mbalimbali ya huduma kwa wanachama wa NHIF na namna ambavyo Jeshi hilo linaweza kunufaika na maboresho hayo.
Katika picha Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dkt. Irene Isaka akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Magereza makao makuu, baada ya kufanya mazungumzo juu ya maboresho mbalimbali ya kihuduma yalifanywa na Mfuko ikiwemo ya huduma za ziada (Supplimentary Package)
Ujumbe kutoka Jeshi la Magereza uliongozwa na SACP. N. Mwankenja aliyeambatana na SP. A. Kachima.
Ujumbe wa Jeshi la Magereza umefurahishwa na maboresho yaliyofanywa na Mfuko ikiwemo wigo wa huduma za ziada ( supplimentary services) kwa wanachama wanaohitaji.