JAJI KIONGOZI AIPONGEZA NHIF KWA KURAHISISHA HUDUMA KUPITIA MIFUMO

Imewekwa: 28 January, 2025
JAJI KIONGOZI AIPONGEZA NHIF KWA KURAHISISHA HUDUMA KUPITIA MIFUMO

Mhe. Jaji Kiongozi Mustapher Mohamed Siyani amepongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuendelea kuboresha huduma zake hususan huduma kwa  wanchama ambapo sasa mwanachama ataweza kujisajili kwa njia ya mtandao. 

Amezungumza hayo leo Januari 28. 2025 alipotembelea banda la NHIF katika Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Alisisitiza kuwa huduma ya bima ya afya ni muhimu sana na inatakiwa iwafikie mpaka watu wa vijijini kwa kuwapatia elimu ili waweze kujiunga na huduma hii. 

“Niwapongeze kwa kuendelea kurahisisha namna ambavyo mwanachama anaweza kupata huduma za bima ya afya katika simu yake ya kiganjani. Tunaangalia na kuona jinsi gani Mfuko huu unavyoendelea kufanya kazi nzuri kwa manufaa ya Watanzania wote” Alisema Mhe. Siyani. 

Naye kwa upande wake Afisa Uhusiano wa NHIF Bw. Charles Madangi alielezea maboresho ya mfumo yaliyofanywa na NHIF hususan katika eneo la usajili wa wanachama na kumshukuru Mhe . Jaji Kiongozi kwa kutembelea banda la NHIF.