Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw. Eliud Sanga amewataka Watumishi kujiepusha na vitendo vya udanganyifu wakati wanapotimiza majukumu yao.
Akizungumza na Watumishi wa NHIF Mkoa wa Mtwara ambapo Bodi imefanya ziara, alisisitiza watumishi kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili wanachama wapate huduma bora na ya haraka.
Alitumia fursa hiyo pia kuwataka kuwa wabunifu kwa kusoma mazingira wanayoishi wananchi wa Mtwara na kuzingatia mila na desturi zao ili kuwezesha wananchi hao kuona umuhimu wa bima ya afya na kujiunga.
Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali. Patrick Kenan Sawala wa Kutoka Kulia walipomtembelea Ofisi kwake mapema wiki hii.
“Pia tumieni fursa zilizopo mkoani hapa kujiendeleza kielimu na kiuchumi hii itawasaidia kuwa na maendeleo binafsi na kuwapa mazingira rafiki ya kutekeleza majukumu yenu,” alisema Bw. Sanga.
Akizunguza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi, Mkurugenzi Mkuu Dkt. Irene Isaka aliwataka Watumishi kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa katika kutekeleza majukumu yao.
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge sasa