Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imepatiwa mafunzo juu ya mfumo wa malipo kwa watoa huduma unaofahamika kama capitation.
Katika mafunzo hayo, Dkt. Francis Rutalala kutoka TAMISEMI alieleza historia ya Mfumo wa capitation, tangu kuanzishwa kwa majaribio mwaka 1996 hadi kuboreshwa mwaka 2018 kwa kutumia mfumo wa kidigitali wa IMIS. Pia alieleza namna michango ilivyopangwa katika mikoa mbalimbali na faida za Mfuko huo, ikiwemo wananchi kupata huduma za matibabu kuanzia zahanati hadi hospitali za rufaa za mikoa.
Dkt. Rutalala alisisitiza umuhimu wa kushirikiana na serikali za mitaa kusajili wanachama kwa ufanisi.
Alipendekeza pia fedha za bima ziwekwe kwenye kapu moja na malipo kufanyika kila mwezi kulingana na idadi ya wateja.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene C. Isaka, aliwashirikisha uzoefu nchi mbalimbali zinazotumia mfumo wa Capitation na mambo muhimu ya kuzingatia katika capitation kama vile kuhakikisha malipo yanafanyika kwa wakati. usimamizi wa mtiririko wa fedha, chombo cha kusimamia malalamiko, marekebisho ya vihatarishi (risk adjusters), uwepo wa champion, uimarishaji wa ushirikiano/ mtandao wa vituo vya kutolea huduma. Alisema kwa kuanzia, utatatibu wa malipo utakuwa both fee for service and Capitation.
Aidha, alieleza jinsi Menejiment ilivyojipanga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa bima ya afya na kuonesha maandalizi yaliyofanywa na serikali katika kuboresha miundombinu na huduma za afya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bw. Eliud B.Sanga, aliishukuru timu ya mafunzo na kusisitiza kuwa kushirikiana na TAMISEMI itawezesha waliokuwa wanachama wa CHF kuanza kusajiliwa na kuchangia bima ya Afya kwa wote. Huu ni mwanzo mzuri wa utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, alielekeza Menejimenti ya NHIF kuendeleza ushirikiano na TAMISEMI ili kuwafikia wanachama CHF ambao kwasasa hawana Bima ya afya.
Capitation ni mfumo wa malipo ya huduma kwa vituo vya Afya ambayo hufanywa kabla ya kutoa huduma kulingana na idadi ya wagonjwa, aina za magonjwa, jinsia na mahudhurio.
Fee for service na mfumo wa malipo ambao malipo hufanywa baada ya mgonjwa kupata huduma. Kiwango hiki hushuka au kupanda kutegemea na huduma zilizotolewa.
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge sasa