Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dkt. Irene Isaka, amepongeza matumizi ya teknolojia za kidijiti uimarishwaji wa Mfumo wa NEST kwenye ununuzi wa umma kwani kumeongeza uwazi, uwajibikaji, ufanisi na thamani ya fedha za umma.

Dkt Isaka ameyasema hayo Julai 30, 2026 wakati akiongoza mjadala wa mada ya Mageuzi ya Kidigitali katika Ununuzi wa Umma "Digital Transformation of Public Procurement" katika Mkutano wa Kumi ya Mwaka ya Utawala Bora katika Ununuzi wa Umma (The 10th Annual Procurement Governance Workshop 2026) uliofanyika Jijini Arusha.
Aidha, alileza kuwa mageuzi ya kidijiti ni msingi muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma za umma na kuongeza imani ya wananchi kwa taasisi za serikalini. Kwa kutumia mfumo wa NEST, Taasisi zimepunguza matumizi ya karatasi kwa zaidi ya asilimia 90%, muda wa kuchakata Zabuni nao umepungua umepungua. Makundi maalum zaidi ya 24,000 yamesajiliwa. Hayo ni mafanikio makubwa. Sasa kinachofuata ni kujenga uwezo wa Taasisi nunuzi pamoja na makundi hayo ili kuweza kupata fursa ya 30% iliyotengwa kwa mujibu wa sheria...alisema Dkt Isaka
_1785692215.jpeg)
Mkutano huo umewakutanisha Viongozi wa Taasisi za umma, wataalamu wa ununuzi, Bodi za zabuni, wakuu wa vitengo vya Ununuzi, wadau wa maendeleo na sekta binafsi kujadili mbinu bora za kuimarisha utawala katika ununuzi wa umma kupitia matumizi ya teknolojia na mifumo ya kisasa, sambamba na kubadilishana uzoefu unaolenga kuongeza tija na ufanisi katika usimamizi wa rasilimali za umma.
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!
_1785692151.jpeg)
_1785692181.jpeg)