BODI YA WAKURUGENZI YA NHIF YARIDHISHWA NA KASI YA UTENDAJI:

Imewekwa: 24 August, 2025
BODI YA WAKURUGENZI YA NHIF YARIDHISHWA NA KASI YA UTENDAJI:

Dodoma   

Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imekutana katika kikao cha kwanza kwa mwaka wa fedha 2025/26 mnamo tarehe 22 Agosti 2025 Jijini Dodoma, makao makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF. Kikao hicho kilijadili ripoti ya maendeleo ya utendaji wa Mfuko kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Bw. Eliud B. Sanga, kilipitia taarifa mbalimbali za Mfuko zikiwemo taarifa toka Kamati ya Ukaguzi, Kamati ya Fedha na Uendeshaji na Kamati Maslahi na Maendeleo ya Watumishi. 

Taarifa hiyo ilionesha:

 1) kuongezeka kwa thamani ya rasilimali za Mfuko kwa asilimia 22.91 kati ya  mwezi Julai, 2024 hadi mwezi Juni, 2025;

2) Ongezeko la ziada ya mapato (surplus) kwa asilimia 300.78 ziada hii imesaidia Mfuko kulipa  madai ya watoa huduma na hivyo kupunguza malalamiko. Muda wa malipo umepungua kutoka siku 120 mwaka 2023/24  hadi siku 50 mwaka 2024/25. Hayo ni

mafanikio makubwa ikilinganishwa na matakwa ya kisheria kulipa madai ndani ya siku 60;

 3) Ongezeko la (reserve) kwa asilimia 34.33 kati ya mwaka wa fedha 2023/24 na mwaka 2024/25; ongezeko hilo limewezesha Mfuko kutengeneza vifurushi vya (Tarangire, Mikumi, Ngorongoro,  Serengeti na Tanzanite) na hivyo kupunguza gharama za matibabu kwa wanachama, ikiwemo wanawake na watoto na  hata wale wenye magonjwa sugu yasiyoambukiza (NCDs);

4) Kuimarika kwa uhimilivu wa Mfuko (sustainability) toka miezi sita mwaka 2024 hadi uhimilivu miezi ishirini na nne yaani miaka miwili(funding level of 2yrs)  mwaka 2024/25;

5) Utekelezaji wa mradi wa TEHAMA kwa kutumia wataalam wa ndani ambapo kwa mwaka 2024/25 Mfuko umeokoa kiasi cha Shilingi bilioni 3.5,
mradi huu umepunguza matumizi ya karatasi (Claim forms) kwa 75%  kutokana na kuchakata madai kupitia mifumo. Pia mradi umepunguza gharama za Kadi za wanachama kwa 80%. Hivi sasa wanachama  wanatumia kadi za kielektroniki (e-card), 
mradi huo pia umeboresha huduma kwa wanachama kupitia huduma ya NHIF Jihudumie (NHIF Self-Service) ikiwemo 

Kuchakata madai kidigiti  umeongeza ufanisi na kupunguza vitendo vya udanganyifu.

Mafanikio makubwa ya mradi huo wa TEHAMA yaliwezesha kupata tuzo ya mshindi wa pili kati ya miradi bunifu ya TEHAMA kitaifa kwa mwaka 2024/25;

6) katika kikao hicho Bodi ilipongeza jitihada za Mfuko kupambana na udanganyifu ambapo kwa mwaka 2024/25 Mfuko ulifungia vituo mbalimbali ambavyo vilijihusisha na udanganyifu.  Aidha, Mfuko ulipeleka orodha ya majina 19 ya Wataalam wa afya waliojihusisha na udanganyifu kwenye mabaraza yao ya kitaaluma kwa hatua zaidi.  Zaidi ya hapo,
Mfuko ulikusanya
 91% ya fedha kutokana na vitendo vya udanganyifu. 
 Pamoja na pongezi hizo Bodi aliagiza Menejimenti kutovumilia vitendo vyovyote vya vya udanganyifu yaani (zero tolerance);

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Dkt. Irene C. Isaka, akielezea jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na Menejimenti ili kuongeza ufanisi wa Mfuko alisema:

1) Kwa mwaka wa fefha 2024/25 Mfuko ulifanya jitihada kubwa ya kubana matumizi kwa kuelekeza rasilimali za Mfuko kwenye maenei yenye tija zaidi, hatua iliyopelekea uwiano wa matumizi na mapato ya Mfuko kuimarika;

2) Dkt Isaka aliendelea kusema, katika kipindi hicho 2024/25 Mfuko ulifanya zoezi la uchambuzi wa majukumu ya kila kada (workload analysis) kwa lengo la kufanya mgawanyo wa majukumu kwa uwiano sahihi, zoezi hilo limekamilika na utekelezaji unaendelra kama Bodi ilivyoelekeza;

3) Ili kuendelea kuwajengea uwezo Watumishi Dkt. Isaka alisema kwa mwaka wa fedha 2024/25 Watumishi wote walihudhuria mafunzo ya muda mfupi yaliyolenga kujenga ujuzi (skills enhencement programs) ili kuongeza tija kwa Mfuko;

) Kwa upande wa utekelezaji wa sera ya magonjwa sugu yasiyoambukiza (NCDs) Dkt. Isaka alisema, Mfuko unafanya jitihada mbalimbali zenye kuwezesha Watumishi kuepukana na maradhi sugu yasiyoambukiza kwa kuwezesha Watumishi kushiriki mafunzo, mazoezi, michezo na mashindano mbalimbali ikiweno mashindano ya?SHIMMUTA, mbio za marathon, mafunzo ya afya ya akili na uwepo wa eneo la mazoezi kwa Watumishi wa Makao Makuh (GYM);

5) Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu alisema Mfuko unaendeke kutekeleza mkakati wa kupambana na rushwa pamoja na mkakati wa kupambana na ukimwi ikiwa ni matakwa ya mikakati ya kitaifa;

6) Dkt. Isaka pia alitumia wasaa huo kuifahamisha Bodi kuwa Mfuko upo katika mwaka wa mwisho wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mfuko (strategic plan)  wa miaka mitano, kuwa mkakati huo umeshafanyiwa tathmini ya utekelezaji wake, hatua itakayosaidia  kwenye maandalizi ya Mkakati mpya;

7) Mkurugenzi Mkuu pia, alielezea mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato ya Mfuko kwa kusajili wanachama wengi zaidi toka makundi mbalimbali wakiwemo wakulima, wafugaji, wachimbaji wadogo wa madini, wavuvi, wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja na makundi mengine, alisema mpaka sasa Mfuko umeingia makubaliano na Mrajis wa Vyama vya Ushirika kupitia (TCDC) kwa ajili ya kushirikiana kusajili wanachama toka vyama vya ushirika nchini. Jitihada nyingine iliyofanyika ni Mfuko kuingia makubaliano na Chama cha Mawakala wa Bima Nchini, kwa lengo la  kusajili wanachama wa sekta isiyo rasmi hasa wafanyabiashara wadogo wadogo kote nchini;

Baada ya maelezo yake, Dkt. Isaka alimshukuru Mwenyekiti wa Bodi na Wajumbe wote wa Bodi kwa miongozo  na uongozi mahiri wanaotoa kwa Menejimenti ya Mfuko. "Tunajisikia fahari kuwa chini ya Bodi hii yenye Wajumbe mahiri na wenye maono makubwa kwa maendeleo ya Mfuko" alisema Dkt. Isaka.

Baadhi ya wajumbe wa menejimenti wakifuatilia kikao cha Bodi ya kilichofanyika jijini Dodoma tarehe 22 Agosti,2025 katika ukumbi wa NHIF.

Kwa upande wa Wenyeviti wa Kamati, Wenyeviti hao pamoja na pongezi walisisitiza yafuatayo;

1) Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi CPA. Veronica Kashala alielezea nia ya Serikali kulipa deni lake la Shilingi bilioni 181 kupitia hati fungani isiyo taslimu ( non cash bond) hali itakayowezesha uwezo wa Mfuko kuimarika zaidi, pia CPA Kashala aliipongeza Menejimenti kwa namna inavyoshughulikia hoja za ukaguzi toka kwa CAG, BOT na PPRA.

2) Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uendeshaji Prof. George Ruhago alisisitiza Mfuko kuutangazia Umma mafanikio na hatua mbalimbali zinazofanyika ili wanachama na wadau waweze kufahamu huduma na maboresho mbalimbali yanayofanywa na Mfuko. "Mfuko unafanya mambo mengi mazuri, muhimu ni kuhakikisha umma unafahamu" alisema Prof. Ruhaga.
Vile vile alisisitiza kwamba pamoja na mwanzo mzuri, wadau wana matarajio makubwa zaidi hivyo tusirudi nyuma.

3) Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maslahi na Maendeleo ya Watumishi. Prof. Kaushik Rumaiya alisema, pamoja na mafanikio yaliyopatikana Mfuko uendelee kufanya mikutano ya mara kwa mara na wadau kwa ajili ya mijadala yenye lengo la kuboresha utendaji kwa pande zote. Pia alisisitiza kuwa Mfuko uweke mkazo wa uwepo wa afua (interventions) za kuzuia maradhi sugu yasiyoambukiza kuliko kusubiri hatua ya kutibu, alisema hatua hii ni muhimu sana kwakuwa itapunguza sana gharama kwa Mfuko.

Wajumbe wengine wa Bodi waliohudhuria kikao hicho ni Ms. Zubeda Mpinga na CPA Dickson Kaambwa.

Pia Wajumbe hao wakitoa michango yao walisema:

1) Ms. Zubeda Mpinga alitoa angalizo muhimu la kulinda taarifa mbalimbali za wanachama hasa wakati wa Actuarial valuation.  "Taarifa ni bidhaa muhimu sana kwa dunia ya sasa, hivyo ni muhimu kwa Mfuko kuhakikisha kuwa taarifa zinalindwa kwa mujibu wa Sheria na Miongozo" alisema Ms. Mpinga.

2) CPA. Dickson Kaambwa kwa upande wake alisisitiza Mfuko kufuata mwongozo wa Udhibiti Majanga (risk guidelines) ili kwenda sambamba na Sera za nchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi Bw. Eliud B. Sanga, alipongeza kwa mafanikio mbalimbali ambayo Mfuko umeoata kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2024/25. Maeneo muhimu aliyopongeza ni:

1) Kuimarika kwa ustahimilivu wa Mfuko;

2) Kuongezeka kwa (reserve) ya Mfuko;

3) Kuongezeka kwa ziada ya mapato ya Mfuko (surplus);

4) Mchanganyiko mzuri wa maeneo ya uwekezaji (investmdnt portfolio), unaowezesha Mfuko kuweza kumudu kutumiza wajibu ( obligations) zake kwa wakati (liquidity);

5) Mafanikio taliyotokana na mradi wa TEHAMA ikiwemo mradi kupata tuzo ya mradi bunifu kwa mwaka 2024/25.

Mwenyekiti alimaliza kwa kusisitiza kuwa, Menejimenti na Watumishi wote tuendelee kufanya kazi kwa bidii ili kuendelea kuongeza mapato na uwezo wa Mfuko. "Mkiendelea kufanya hivyo, Bodi itakuws mstari wa mbele katika kuhakikisha maslahi ya Watumishi yanaboreshwa" alissma Bw. Sanga.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko,  Dkt. Isaka  akimalizia kwa kusema, Menejimenti imepokea kwa unyenyekevu pongezi za Bodi, na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Bodi, ikiwemo kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kufikia malengo yaliyowekwa kwa ustawi wa Mfuko na Wanachama.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa